20. Njooni wachungaji Betlehemu

1 Njooni wachungaji Betlehemu!
Njooni kumtazama mtoto mzuri.
Mwana wa Mungu amezaliwa.
Baba amtuma awakoboe.
Msiogope!

2 Twende Betlehemu tuone
tulivyoambiwa na malaika.
Tuyaonayo tutatangaza
na kutukuza kwa nyimbo nzuri.
Haleluya!

3 Kweli malaika wametangaza
Furaha kubwa kwa wachungaji.
Sasa popote patengenezwe,
na watu wote watapendezwa.
Furahini!

Text Information
First Line: Njooni wachungaji Betlehemu!
Title: Njooni wachungaji Betlehemu
German Title: Kommet ihr Hirten, ihr Männer und Frauen
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuzaliwa kwa Yesu
Notes: Sauti na wimbo: Kommet ihr Hirten, ihr Männer und Freuen; Asili: Bohemia, 1870, Grosse Missionsharfe, Erster Band #34, Tumwimbie Bwana #16
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us