Text: | Bwana Yesu yuko wapi |
1 Bwana Yesu yuko wapi,
mpenzi wangu, rafiki?
Njia gani amekwenda?
Nitamwonaje mimi?
Roho yangu yajutishwa
na dhambi na huzuni;
Yesu mpenzi wangu mwema
namtafuta kwa bidii.
2 Napaliza sauti yangu
nalia: Wapi Yesu?
Ndani mwangu sina raha
mpaka nimwone Yesu.
Ningekuwa na mabawa
ningeruka upesi
milimani, mabondeni
kumtafuta Bwanangu.
3 Aondoa shida zangu,
maharibifu yote.
Nikiona taabu mimi
anituliza yeye.
Nitafanya bidii sana;
kumtafuta popote;
sitachoka kutembea
mchana hata usiku.
4 Bwana Yesu nitokee,
roho inakuita.
Niondoe na maovu
Yesu Mwokozi wangu.
Utulize hamu yangu
kaa kwangu daima.
Nikupende sana wewe,
niwe wako milele.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Bwana Yesu yuko wapi |
Title: | Bwana Yesu yuko wapi |
German Title: | Wo ist Jesus, mein Verlangen |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kujuta na kutegemea: Kujuta |
Notes: | Sauti: Kijerumani, Asili, Silesia, 1819, Grosse Missionsharfe #151, Nyimbo za Kikristo #217 |