Text: | Ukiwa na ubaya |
1 Ukiwa na ubaya
umwambie Bwana!
Ukishindana nao,
atakutakasa.
Damu aliyotoa,
ndiyo itoshayo,
kuosha wakosaji,
hata wewe vivyo.
2 Vilevile na moyo
umtolee Bwana!
Ndivyo vipaji vema
vinavyompendeza.
Kwani sisi wenyewe
alitukomboa,
akiuawa yeye
kwa kuwambwa mtini.
3 Hata viwe vichache
umtolee Bwana,
vyote tulivyo navyo
vimetoka kwake.
Vipaji vyako habe
yeye hakatai,
kidogo kwako wewe,
kwake kitazidi!
4 Vitu vya mali nyingi
umtolee Bwana!
Alitoka mbinguni
kusumbuka hapa.
Alikufa mwenyewe
kwa ajili yako,
nawe hutoi chako
kwa ajili yake?
5 Wakristo na tutoe
shukrani kwa Mungu!
Hiyo ndiyo shukrani
ya wokovu wetu.
Injili yake Kristo,
Ienee pote!
Kwa ushuhuda wetu
watu waokoke.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Ukiwa na ubaya |
Title: | Ukiwa na ubaya |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kuteswa na kufa kwa Yesu |
Notes: | Sauti: S. Salvatori, nyimbo za Kikristo #73, Hymnal Companion #96 |