94. Bwana Yesu alikufa

1 Bwana Yesu alikufa
kwa sababu yetu sisi,
alipata duniani
maumivu mengi sana.

2 Bustanini akiomba
akafadhaika kabisa.
Jasho lake kama damu
nchini ikadondoka.

3 Wayuda wakamwendea,
wakamshika, wakamfunga.
Na rafiki zake wote
wakimbia, wkamwacha.

4 Na wale wakampeleka
barazani kumhukumu.
Wamhukumu yule mfalme,
atakayewahukumu.

5 Wakamfyosa, wakampiga,
wakampeleka Golgota.
Kule wakamwamba mtini,
kwa misumari kumkaza.

6 Kukawa na giza huko,
na nchi ikatetemeka.
Watu walioko wote,
wakaona woga mwingi.

7 Na saa tisa ikifika
Yesu apaza sauti kuu,
kwamba: Yamemalizika;
mara akakata roho.

8 Askari wakamwendea,
wakamwona amekufa.
Nao wakamchoma mkuki;
ukapenya moyo wake.

9 Damu yaki ikatoka,
yakatoka maji tena,
Maji, damu iwezago
kuosha uchafu wote.

10 Na watu wema wamshusha,
wamfunga katika sanda,
wakamweka kaburini,
na penye mlango jiwe kuu.

11 Siku ya tatu atoka
Yesu Kristo kuzimuni,
alivyotangaza kwanza.
Ye mzima hata milele!

Text Information
First Line: Bwana Yesu alikufa
Title: Bwana Yesu alikufa
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuteswa na kufa kwa Yesu
Notes: Sauti: Rockingham by E. Miller, Reichs Lieder #423, Hymnal Companion #36, Lutheran Book of Worship #482
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us