99. Mungu tusaidie

1 Mungu tusaidie,
Sisi tunaangamia.
Nchi imeharibika
Na mwovu wake Shetani.

Refrain:
Kweli kweli ndiye Yesu
Aliyewambwa mtini
Penye mlima wa Golgotha
Aokoe wenye dhambi.

2 Kaonyesha huruma,
Wayuda wakasumbua.
Wakampiga makofi,
Pilato aliamua. [Refrain]

3 Yesu mwenye upendo
Alikubali kuuawa,
Damu ilimwagika
Ili sisi tuokoke. [Refrain]

4 Pale msalabani,
Bwana Yesu aliteswa
Mzigo wa dhambi zetu
Ulimwangukia yeye. [Refrain]

5 Sote na tukumbuke,
Kifo cha Mwokozi wetu.
Alisema ya kwamba
Jililieni wenyewe. [Refrain]

6 Habari zilisemwa,
Mahali hapa hayupo,
Ona alipokuwa,
Jiwe limeondolewa. [Refrain]

7 Ni ajabu kabisa
Wingu kuja kumpokea.
Habari ilisema
Yesu atarudi tena. [Refrain]

Text Information
First Line: Mungu tusaidie
Title: Mungu tusaidie
Refrain First Line: Kweli kweli ndiye Yesu
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuteswa na kufa kwa Yesu
Notes: Suati: Kinyakyusa
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us