Author: N. Selnecker, 1532 (1530)-1592 Hymnal: Mwimbieni Bwana #243 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Sikukuu za Wakristo Lyrics: 1 Kristo usituondoke
sababu mchana waisha,
mwanga wa Neno la Mungu
usiuzimishe kwetu!
2 Nyakati hizi za mwisho
tusaidie kushika
neno la huruma yako
nalo fumbo takatifu.
3 Kundi lako ulilinde
ulikusanye mwenyewe,
libariki neno lako,
litangaziwe popote!
4 Mambo na mashauri yote
si yetu ila ni yako,
kwa hiyo wasimamishe
wanaokutegemea.
5 Neno lako ngome kubwa,
hata boma la makundi:
kwa neno lako tulishe,
tusitafute mengine! Languages: Swahili
Kristo usituondoke