Author: J. L. K. Allendorf Hymnal: Mwimbieni Bwana #64 (1988) Topics: Epifania, Mission Lyrics: 1 Yesu ni mponya,
aleta furaha!
Mwanzo na mwisho
wa vyote ndiye.
Mwana Adamu
na Mungu wa kweli
ametujia atubariki.
Mbingu, dunia,
toeni habari:
Yesu ni mponya,
aleta furaha!
2 Yesu ni mponya,
aleta wokovu!
Sikilizeni habari njema!
Sisi tulipomwacha
Mungu wetu
akaturudisha tena kwake.
Ametufanya watoto
wa Mungu.
Yesu ni mponya,
aleta wokovu.
3 Yesu ni mponya,
aleta uzima!
Kamba za kufa zimekatika.
Mwana wa Mungu
kamshinda Shetani,
awakomboe watumwa
wake,
amewapata, kawapa uhuru.
Yesu ni mponya,
aleta uzima.
4 Yesu ni mponya,
mchungaji wa kweli,
anayelisha vizuri kondoo.
Wote walio mbali awaita,
awarudishe kundini
mwake.
Awakomboa
kondoo kufani:
Yesu ni mponya,
mchungaji wa kweli.
5 Yesu ni mponya
na mfalme wa enzi!
Mbingu zimsifu
na watu wamtii.
Anageuza mioyo ya watu,
hata na sisi na tumpe yetu,
kwani apenda
kutupa uzima.
Yesu ni mponya
na Mfalme wa enzi!
6 Yesu ni mponya
na mwenye upendo!
Anatupenda
kwa moyo wote.
Yeye mwenyewe
upendo wa kweli,
aliyekufa kwa kutupenda.
Nasi tumpende kwa nguvu
ya roho!
Yesu ni mponya na mwenye
upendo! Languages: Swahili
Yesu ni mponya