Text Results

Topics:kuteswa+na+kufa+kwa+yesu
In:texts

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 1 - 10 of 24Results Per Page: 102050
Text

Bwana Yesu alikufa

Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Bwana Yesu alikufa kwa sababu yetu sisi, alipata duniani maumivu mengi sana. 2 Bustanini akiomba akafadhaika kabisa. Jasho lake kama damu nchini ikadondoka. 3 Wayuda wakamwendea, wakamshika, wakamfunga. Na rafiki zake wote wakimbia, wkamwacha. 4 Na wale wakampeleka barazani kumhukumu. Wamhukumu yule mfalme, atakayewahukumu. 5 Wakamfyosa, wakampiga, wakampeleka Golgota. Kule wakamwamba mtini, kwa misumari kumkaza. 6 Kukawa na giza huko, na nchi ikatetemeka. Watu walioko wote, wakaona woga mwingi. 7 Na saa tisa ikifika Yesu apaza sauti kuu, kwamba: Yamemalizika; mara akakata roho. 8 Askari wakamwendea, wakamwona amekufa. Nao wakamchoma mkuki; ukapenya moyo wake. 9 Damu yaki ikatoka, yakatoka maji tena, Maji, damu iwezago kuosha uchafu wote. 10 Na watu wema wamshusha, wamfunga katika sanda, wakamweka kaburini, na penye mlango jiwe kuu. 11 Siku ya tatu atoka Yesu Kristo kuzimuni, alivyotangaza kwanza. Ye mzima hata milele!
TextPage scans

Yesu, kuteswa kwako

Author: S. V. Birken, 1626-1681 Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Yesu, kuteswa kwako nitakufikiri. Nipe kwa shauri hili roho na mbaraka. Moyo wangu uone hali yako Yesu, jinsi ulivyoteswa kwa ajili yetu. 2 Moyo wangu uone taabu yako kubwa, maumivu, mapigo, na kuwambwa mtini, taji lako la miiba tena misumari, iliyokuumiza, hata kufa kwako. 3 Nikitazama yote yaliyokutesa, nifikiri sababu na maana yake. Sababu ndio mimi na makosa yangu: umepata mateso, nipate huruma. 4 Yesu unifundishe nijute kwa moyo; nisikuzidishie shida na uchungu. Nisiweze kupenda yaliyokutesa: nataka kuyaacha na kukufuata.

Mungu ameona tulivyo

Author: Y. Chambile Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mungu ameona Refrain First Line: Ya kwamba Yesu kaja
TextPage scans

Nakusalimu kichwa

Author: Bernhard V. Clairvaux, 1091-1153; Paul Gerhardt, 1607-1676 Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nakusalimu kichwa kilichojaa damu, kilichovikwa taji la miiba mikubwa, kilichopata enzi kwa Mungu mbinguni, kitukanwacho sasa matusi makali. 2 Naona uso wako watemewa mate, heshima yako yote imeondolewa. Mwanga wa macho yako wazimika sasa. Aliyekuharibu hivi, ndiye nani? 3 Mateso yako Bwana, yanipasa mimi. Wewe waadhibishwa kwa ajili yangu. Hukumu unapata iliyonipasa. Bwanangu nakuomba, unihurumie! 4 Na mimi nasimama msalabani pako; niwe karibu kwako utoapo roho; ukiugua sana kwa teso la kufa, nitakushika Bwana kwa moyo wa pendo. 5 Bwana nayashukuru masumbaku yako, sababu ya kuteswa na kufa kuchungu. Wewe umenishika, nami nakushinka, mwisho nitakufia uliyenifia. 6 Moyo unaposhikwa na woga wa kufa, usiniache Bwana katika vita hii. Siku ya kufa kwangu unisaidie, kufa kwako kuchungu kutaniokoa. 7 Niwie kama ngao nitakapokufa, nione uso wako katika uchungu. Ndipo nikutazame nikukumbatie! Anayekufa hivi afa kwa amani.
TextPage scans

Nataka kusimama

Author: E. C. Clephane, 1830-1869 Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nataka kusimama chini ya msalaba, kama kivuli cha mwamba wakati wa mchana, kama ni maji nyikani, kambi safarini, na hapa nitapumzika, kwani jua kali. 2 Mahali pema sana chini ya msalaba, kwani hapo waoneka upendo wa Yesu. Yakobo alivyoona ndotoni zamani, mti Yesu aliowambwa, ni ngazi kwa Mungu. 3 Juu ya msalaba huo Yesu alikufa. Alikufa tuokoke, tuliopotea. Ninastaajabu kabisa ni mambo mawili: kwake Yesu ni upendo, kwangu mimi kosa! 4 Wataka kuonana na Yesu mbinguni, yakupasa kukaa kwanza chini ya mti huo. Ni kweli siku chache tu mateso na shaka. Halafu pasipo mwisho furaha kwa Bwana!
TextPage scans

Ukiwa na ubaya

Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ukiwa na ubaya umwambie Bwana! Ukishindana nao, atakutakasa. Damu aliyotoa, ndiyo itoshayo, kuosha wakosaji, hata wewe vivyo. 2 Vilevile na moyo umtolee Bwana! Ndivyo vipaji vema vinavyompendeza. Kwani sisi wenyewe alitukomboa, akiuawa yeye kwa kuwambwa mtini. 3 Hata viwe vichache umtolee Bwana, vyote tulivyo navyo vimetoka kwake. Vipaji vyako habe yeye hakatai, kidogo kwako wewe, kwake kitazidi! 4 Vitu vya mali nyingi umtolee Bwana! Alitoka mbinguni kusumbuka hapa. Alikufa mwenyewe kwa ajili yako, nawe hutoi chako kwa ajili yake? 5 Wakristo na tutoe shukrani kwa Mungu! Hiyo ndiyo shukrani ya wokovu wetu. Injili yake Kristo, Ienee pote! Kwa ushuhuda wetu watu waokoke.
TextPage scans

Mungu tusaidie

Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Refrain First Line: Kweli kweli ndiye Yesu Lyrics: 1 Mungu tusaidie, Sisi tunaangamia. Nchi imeharibika Na mwovu wake Shetani. Refrain: Kweli kweli ndiye Yesu Aliyewambwa mtini Penye mlima wa Golgotha Aokoe wenye dhambi. 2 Kaonyesha huruma, Wayuda wakasumbua. Wakampiga makofi, Pilato aliamua. [Refrain] 3 Yesu mwenye upendo Alikubali kuuawa, Damu ilimwagika Ili sisi tuokoke. [Refrain] 4 Pale msalabani, Bwana Yesu aliteswa Mzigo wa dhambi zetu Ulimwangukia yeye. [Refrain] 5 Sote na tukumbuke, Kifo cha Mwokozi wetu. Alisema ya kwamba Jililieni wenyewe. [Refrain] 6 Habari zilisemwa, Mahali hapa hayupo, Ona alipokuwa, Jiwe limeondolewa. [Refrain] 7 Ni ajabu kabisa Wingu kuja kumpokea. Habari ilisema Yesu atarudi tena. [Refrain]
Text

Yesu alitufia

Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Yesu alitufia, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 2 Sisi watu wabaya, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 3 Walimchezea Bwana, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 4 Wakamvua mavazi, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 5 Aliteswa Golgotha, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 6 Kasema imekwisha, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 7 Hakushindwa na kifo, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 8 Katoka kaburini, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 9 Kafufuka kwa wafu, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 10 Ndiye Mwokozi wetu, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 11 Ataishi milele, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi.
TextPage scans

Mwana knodoo ayalipa

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mwana kondoo ayalipa Lyrics: 1 Mwana kondoo ayalipa madeni ya dunia. Ayachukua makosa ya wakosaji wote. Aenda na kuugua, anakubali kuchinjwa, furaha aziacha. Wanamhukumu wampiga, wanamukana, wanamtesa, asema: Nakubali. 2 Mwana kondoo ni Mwokozi ni mponya wa mioyo, aliyetumwa na Mungu awakomboe watu Mwanangu, nenda okoa watoto niliotupa, sababu ya makosa. Dhambi zao ni nyingi mno; watolee ukombozi damu na mwili, wako. 3 "Tayari mimi, Babangu, nitwishe nichukue. Maneno uyasemayo nitafuata yote." Pendo hili kubwa sana, lamshika Baba wa mbingu amtoe mwana wake. Pendo hili lina nguvu, linamlaza kaburini aletaye uzima. 4 Sitasahau pendo hili Bwanangu siku zote. Nitakushika daima, kama unishikavyo. Mwanga wa roho ni wewe; roho inapozimia niwie moyo wangu. Na tuagane, Bwanangu, niwe mali yako sasa na halafu mbinguni.

Wakristo twabeba nini?

Author: Z. D. Mzengi Appears in 1 hymnal Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu

Pages


Export as CSV