1 Ewe Bwana ndiwe
mchunga wangu mwema.
Sitapungukiwa na kitu,
Kwani u pamoja nami.
2 Wanilaza kwenye
malisho tele;
Wanitangulia vizuri,
Kwani wanipenda sana.
3 Nafsi yangu
imehuishwa nawe,
Na kuongozwa kwa haki,
Kwa ajili ya jina lako.
4 Nikipitia hata
bonde la mauti,
Sitaogopa mabaya,
Kwani Wee u gongo langu.
5 Umeandaa meza
mbele yangu mimi,
Ili na watesi waone,
Kwamba ndiwe
mwenye neema.
6 Kichwa changu
kimepakwa na mafuta.
Kombe langu linafuika;
Haya umefanya yote.
7 Wema wako
umenifuata hasa.
Nami nitaishi na Wewe,
Kwako, Bwana siku zote.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #273