1 Haya ee moyo wangu,
imba kwa furaha.
Umwimbie Mwumbaji
mbingu na dunia.
Atukuzwaye pote
umsifu na wewe
kwa nguvu zako zote,
umri wako wote.
2 Mungu wake Yakobo,
ndiye Mungu wetu.
Ukimchagua yeye,
una fungu jema,
unacho kitu chema,
umepata mali;
moyo utakung'aa
shida zitakwisha.
3 Ni mwenye nguvu nyingi,
hana amshindaya.
Kwa hekima aumba,
vyote ni ajabu,
misitu na mabonde,
milima, mashamba,
vilivyo baharini
wanyama porini.
4 Ana mizungu mingi,
kuponya wanawe.
Anawapa riziki,
hata siku za njaa.
Wenye chakula haba
wanenepa miili:
hata waliofungwa
anawafungua.
5 Mashangilio yote,
hayamtoshi yeye.
Ni mwema peke yake
nami ni vumbi tu!
Ananihurumia
kwa kuwa ni wake,
kwa hiyo nalikuza
jina lake pote.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #256