1 Mwokozi wangu, umekosa nini?
Wahukumiwa kama mwuaji.
Umeshtakiwa makosa mangapi
uliyotenda?
2 Wapigwa sana, miiba taji lako,
umetemewa mate, watukanwa,
wanyweshwa nyongo,
tena siki kali, wasulibishwa!
3 Sababu gani unateswa hivi?
Makosa yangu yanakuumiza;
mateso haya yako yanipasa,
mimi mkosaji.
4 Ajabu kubwa sana tendo lako:
Mchungaji unateswa kwa ajili
ya kondoo, Bwana unawalipia
watumwa wako.
5 Tulipokuwa mateka ya mwovu,
nawe ukaja ukatukomboa.
Twalistahili kufa kwa milele,
ukatufia.
6 Mwokozi wangu nifanyeje mimi,
niitangaze pote sifa yako?
Nakufuata nikutumikie
maisha yote.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #77