13. Salamu, Yesu Bwanangu

1 Salamu, Yesu Bwanangu
wewe uzima wangu.
Nimekujia, naleta
vyote ulivyonipa:
Ni moyo na nwili wangu,
hata na mawazo yangu
ndiyo heshima yangu.

2 Umezaliwa Bwanangu
kwa ajili ya mimi;
umenipenda kabisa,
umenipa wokovu.
Tangu mimi sijaumbwa
umenitengenezea
Ukombozi wa moyo.

3 Uvuli mzito wa mauti
ulinifunikiza:
Umenitokea jua,
waniangaza moyo.
Wewe Bwana umenipa
nuru, raha na uzima.
Nakushukuru Bwana.

Text Information
First Line: Salamu, Yesu Bwanangu
Title: Salamu, Yesu Bwanangu
German Title: Es iist gewisslich
Author: Paul Gerhardt, 1607-1676
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuzaliwa kwa Yesu
Notes: Sauti: Es ist gewisslich by Johann Eccard, 1591, Posaunen Buch, Erster Band #115, Lutheran Book of Worship #321
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us