232. Mungu yupo hapa

1 Mungu yupo hapa,
na tumsujudie,
tumche tukamtumikie.
Yu pamoja nasi,
nyamazeni wote
tumlalamikie Mponya.
Wanaolitaja
jina lake, njooni,
tumpeni sadaka.

2 Mungu yupo hapa,
anayesifiwa
na malaika kila siku.
Wote wanaimba:
Mungu mtakatifu,
aheshimiwe popote.
Ee Mungu sikia
tukikuimbia
na sisi wadogo.

3 Twataka kuacha
mambo ya dunia
na uzuri wake wote.
Mioyo na mapenzi
hata nia zetu
tuankutolea Bwana.
Wewe tu, u Mungu,
anayestahili
sifa za viumbe.

4 Mwokozi ingia,
mioyo yetu yote,
iwe nyumba yako wewe.
Ndiwe Bwana wetu,
utusaidie
Tukupende siku zote.
Tukiwa wako tu
tukae na wewe
tukusujudie!

Text Information
First Line: Mungu yupo hapa
Title: Mungu yupo hapa
German Title: Gott ist gegenwartig
Author: G. Tersteegen, 1697-1769
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Sikukuu za Wakristo
Notes: Sauti: Wunderbarer König, Asili: J. Neander, Bremen, 1680, Posaunen Buch, Erster Band #77, Nyimbo za Kikristo #184, Lutheran Book of Worship #249
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us