276. Leo siku ya Mungu

1 Leo siku ya Mungu
Tuko mbele zake.
Jambo kubwa twa'budu
na kusujudia.
Sasa tutulie mbele
zake Mungu.
Awe asi sote
mioyoni mwetu,
Sasa tutulie mbele
zake Mungu.
Awe asi sote
mioyoni mwetu.

2 Sisi viumbe vyake
tuombe huruma,
Muumba vitu vyote
atahurumie.
Yeye atupenda
na kujua yote.
Manza zetu zote
atazisafisha,
Yeye atupenda
na kujua yote.
Manza zetu zote
atazisafisha.

3 Neno lako la leo
liwe ndani yetu.
Mapenzi yake yote
yatimizwe kwetu.
Tumfuate yeye,
na tuishi naye.
Awe baba yetu
maishani mwote,
Tumfuate yeye,
na tuishi naye.
Awe baba yetu
maishani mwote.

4 Sisi wana wa Mungu,
tuna humu kubwa
Kuwa na neema yake,
Yesu Bwana wetu.
Basi, ndugu sote,
tuwe ndani yake,
Naye ndani yetu,
tumtumikie,
Basi, ndugu sote,
tuwe ndani yake,
Naye ndani yetu,
tumtumikie.

Text Information
First Line: Leo siku ya Mungu
Title: Leo siku ya Mungu
Author: Wilson Kyakajumba
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kujuta na kutegemea: Kujuta
Notes: Asili: Kihaya, Tumshangilie Mungu #56
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us