86. Ee, watoto njooni

1 Ee, watoto njooni,
njooni Golgota,
mtazameni
Yesu aumizwavyo!

2 Mtazameni huko
mkamtazame,
Sogeeni kwake,
ametupenda.

3 Sogeeni kwake,
mkamtazame,
mioyo iyevuke,
mwangukieni!

4 Mioyo imlilie
anayeteswa;
mzigo wetu mkubwa
aukubali.

5 Mzigo wa makosa
ya ulimwengu.
Mpeni nanyi nyote
mioyo yenu!

6 Apata mshahara,
ni kufa kwake;
wewe una raha,
kwake ni kufa.

7 Ataona enzi
ya utukufu.
Tuimbe Haleluya
na kumshukuru!

Text Information
First Line: Ee, watoto njooni
Title: Ee, watoto njooni
German Title: Kommt, o liebe Kinder
Author: E. G. Woltersdorf (1725)
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuteswa na kufa kwa Yesu
Notes: Sauti: Kommt, o liebe Kinder ny E. G. Woltersdorf, 1725, Asili: 1875, Grosse Missionsharfe, Erster Band #24, Nyimbo za Kikristo #68
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us