3. Watu Wa Yesu

1 Watu wa Yesu, sifuni Bwana,
M-tangazeni, ulimwenguni,
Sifa za Yesu, zienee pote,
Mataifa yote, yamsifu Yesu.

2 Humilki pote, mbingu na n-chi,
Ufalme wake, hauna mwisho,
Wote wa mbinguni m-tukuzeni,
Msifuni daima hata milele.

3 Neema yake ni nyingi sana,
Upendo wake ni wa ajabu,
M-linzi, M-chunga,Mwokozi wetu
Mfarifi, Mwombezi na Kiongozi.

4 Fadhili zake zaonekana,
Anavikidhi viumbe vyake,
Vyakula, vinywaji ni vingi kwake,
Mwangaza na mvua atugawia.

5 Sifuni Bwana kamwimbieni,
Anastahili fahari yoge,
Heshima na pendo m-peni Bwana,
Mwokozi Mwombezi na Mfalme Yesu.

Text Information
First Line: Watu wa Yesu, sifuni Bwana
Title: Watu Wa Yesu
Language: Swahili
Publication Date: 1994
Scripture:
Topic: Irada, Sifa Na Injil
Notes: Sauti: O Worship the King (Lyons), Baptist Hymnal 1991 #16, Nyimbo za Sifa #1, Milo wa Ab- Magipo 3/4
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us