Instance Results

Topics:kumtambikia+mungu
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 11 - 20 of 65Results Per Page: 102050
Page scan

Umsifu Mungu ee roho yangu

Author: J. D. Herrnschmidt, 1675-1723 Hymnal: Mwimbieni Bwana #259 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Kumsifu na kumwomba Mungu Languages: Swahili
Page scan

Tumshukuru Mungu

Author: M. Rinckart, 1586-1649 Hymnal: Mwimbieni Bwana #261 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Kumsifu na kumwomba Mungu Languages: Swahili
TextPage scan

Jua likicha linayang'aza

Author: P. Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #208 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Nyimbo za asubuhi Lyrics: 1 Jua likicha linayang'aza mashamba yetu kwa utukufu wa nuru yake yenye neema kuu. Nimelegea maungo usiku; sasa ni macho, naona furaha nikitazama viumbe vyote. 2 Njooni tuimbe tukamtolee Muumba sadaka za mioyo yetu, mambo mazuri tuliyo nayo. Mungu ataka mioyo ya watu, nyimbo za sifa na za kumshukuru, ndizo sadaka zimpendezazo. 3 Kazi ya Mungu ni kila siku kutubariki, kutuongoza, kutukingia hatari nyingi. Sisi twalala, Bana anakesha; tukiondoka, anatung'azia mwanga mzuri wa huruma yake. 4 Mambo ya watu, yote yapita. Mambo ya Mungu yanasimama Neno la Bwana lakaa milele. Atutolea wokovu wa neema, ayaondoa machungu ya kufa, tuwe wazima hapa na huko. 5 Mwenye huruma unisamehe makosa yangu, uyaondoe machoni pako kwa neema yako. Tena naomba: Nilinde vizuri, uniongoze na kunitawala kama mwenyewe unavyopenda. 6 Msiba na shida mwisho zapita: kama twaona mwanga wa jua baada ya mvua mbinguni tena. Raha, uzima, furaha, amani zaningojea mbinguni kwa Mungu: Ninatamani furaha za juu. Languages: Swahili
TextPage scan

Haleluya! Nakusifu

Author: J. Krause, 1701-1762 Hymnal: Mwimbieni Bwana #231 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Sikukuu za Wakristo Lyrics: 1 Haleluya! Nakusifu Mungu uliyenipa leo tena siku yako, ishindayo nyingine, inanifurahisha moyo wangu kabisa. 2 Ninaacha masumbuko; leo siku ya Bwana. Ninamtumikia Mungu, kwa nguvu zangu zote. Leo vyote havifai ila azi ya Mungu. 3 Ubariki neno lako linapohubiriwa, liingie mioyoni, watu wategemee. Nyimbo hata maombi yakufikie Mungu. 4 Unisaidie Bwana, nimalize siku hii kama nilivyoinza nikikutumikia. Mwisho nione kwako sikukuu ya milele. Languages: Swahili
TextPage scan

Mwezi umechipuka

Author: M. Claudius, 1740-1815 Hymnal: Mwimbieni Bwana #229 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Nyimbo za Jioni Lyrics: 1 Mwezi umechipuka na nyota zamulika mbinguni popote. Makonde yote kimya, na kunako mabonde ukungu mzuri unakaa. 2 Dunia imekuwa nchi ya utulivu, ni nyumba ya raha. Viumbe vyenye taabu, waume, wake, wana na watulie usiku. 3 Tukiwa na kiburi, tu wakosaji sana, wapuzi kabisa. Twatunga vya uongo, na maarifa yote yametutenga na Mungu. 4 Utuonyeshe, Mungu, wokovu wa kikweli, tusijidanganye! Tukae duniani kama watoto wema wamtegemeao Baba. 5 Na sasa ndugu zangu, tuende kujilaza kwa jina la Mungu. Atupe usingizi sisi tuliochoka, hata majirani wote! Languages: Swahili
TextPage scan

Ninataka kumwimbia Muntu

Author: P. Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #253 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Kumsifu na kumwomba Mungu First Line: Ninataka kumwimbia Lyrics: 1 Ninataka kumwimbia Mungu kwa furaha kuu. Ninaona kila siku anihurumiavyo. Moyo wake mwenye kweli umejaa upendo tu, abariki kwa wingi wamtumikiao vema. Vitu vyote vyaisha, pendo lake milele. 2 Kama kuku alindavyo watoto hatarini, vivyo Baba anilinda kila siku kwa nguvu. Ndiye aliyeniumba akanipa mwili huu na uzima na roho siku zote mpaka leo. Vitu vyote vyaisha, pendo lake milele. 3 Jinsi hii aliupenda Mungu ulimwengu huu, hata akamtoa mwana, kwa ajili ya watu. Naye Yesu aliteswa akafa kule mtini atuokoe sisi. Tazameni pendo hili! Vitu vyote vyaisha, pendo lake milele. 4 Roho wake mtakatifu ni kiongozi wangu, aniangalia vema niingie mbinguni, Aning'aza moyo wangu kwa tegemeo langu limshindalo Shetani, asiweze kunidhuru. Vitu vyote vyaisha, pendo lake milele. 5 Nikishikwa na huzuni ninajue faraja: Shida na mateso yote mwisho yatageuka. Baada ya kaskazi kali yanakuja masika vivyo baada ya shida napewa furaha kubwa. Vitu vyote vyaisha, pendo lake milele. 6 Pendo lake haliishi Neno hili ni kweli. Basi mimi mtoto wake ninamwomba Babangu: Unihurumie mimi, nikushike kwa nia, nikupende daima, niishipo duniani; na halafu milele nitakaa na wewe. Languages: Swahili
TextPage scan

Haya ee moyo wangu

Author: P. Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #256 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Kumsifu na kumwomba Mungu Lyrics: 1 Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha. Umwimbie Mwumbaji mbingu na dunia. Atukuzwaye pote umsifu na wewe kwa nguvu zako zote, umri wako wote. 2 Mungu wake Yakobo, ndiye Mungu wetu. Ukimchagua yeye, una fungu jema, unacho kitu chema, umepata mali; moyo utakung'aa shida zitakwisha. 3 Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaya. Kwa hekima aumba, vyote ni ajabu, misitu na mabonde, milima, mashamba, vilivyo baharini wanyama porini. 4 Ana mizungu mingi, kuponya wanawe. Anawapa riziki, hata siku za njaa. Wenye chakula haba wanenepa miili: hata waliofungwa anawafungua. 5 Mashangilio yote, hayamtoshi yeye. Ni mwema peke yake nami ni vumbi tu! Ananihurumia kwa kuwa ni wake, kwa hiyo nalikuza jina lake pote. Languages: Swahili
TextPage scan

Namtumaini Bwana tu

Author: C. Sturm, 1740-1786 Hymnal: Mwimbieni Bwana #257 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Kumsifu na kumwomba Mungu Lyrics: 1 Namtumaini Bwana tu ndiye mtuliza moyo. Amkimbiliaye huyu, hatindikiwi nuru. Kwa neno la Bwana Mungu roho itatulia, moyo watengemana. 2 Kila anayekupenda huona msaada wako, akishikwa na mashaka, ntamtuliza moyo. Moyoni mwampenda Mungu hamu itatulia, uchungu hutoweka. 3 Roho yangu usiache kumtumaini Bwana! Waelekevu huona; kwake vitu vyema. Bwana ndiye mwenye nguvu katika shida zote; ni kinga hatarini. 4 Mkononi mwako naweka maisha na uzima. Nakuinulia macho niwapo duniani. Baada ya siku hizi ukanipe kukaa nbinguni kwako Baba. Languages: Swahili
TextPage scan

Tokea nuru ya mchana

Author: Max v. Schenkendorf, 1783-1817 Hymnal: Mwimbieni Bwana #213 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Nyimbo za asubuhi Lyrics: 1 Tokea nuru ya mchana, uamshe mwili na roho kwa mwanga wako mzuri. Tokea nuru ya roho, niimbe wimbo wa sifa wa kumshukuru Mungu. Mwimbieni kwa furaha Mwenye enzi alindaye na kuwabariki watu. 2 Ninakushukuru Mungu kwa moyo wote sababu ya neema yako kubwa. Umenilinda usiku mwili na roho vizuri kwa jeshi la malaika. Nikaweza kuondoka kitandani kwa furaha mwenye nguvu na uzima. 3 Ninakuomba Babangu, uyaondoe makosa, hofu na shida kwangu. Niamke hata rohoni, kwa neema yako na pendo nitakutumikia. Niongoze nifikiri, mambo yangu mbele yako, nipate baraka yako. 4 Ee Yesu, uniongoze nishike njia yako tu maisha yangu yote. Ulinde mwili na roho uangalie mwenendo nisianguke leo. Mpenzi wangu, nifundishe, nikumbuke pendo lako, nisishindwe na dunia. 5 Unitawale kwa roho unionyeshe mwenendo kwenda kwako mbinguni. Unibariki popote katika kazi na raha, nipe riziki yangu. Mpaka mwisho niondoke duniani kwa furaha, nikushukuru mbinguni. Languages: Swahili
TextPage scan

Asabuhi na mapema

Hymnal: Mwimbieni Bwana #218 (1988) Topics: Kumtambikia Mungu Nyimbo za asubuhi First Line: Asubuhi na mapema Lyrics: 1 Asubuhi na mapema nakukaribia, kukushukuru, ee Bwana, kwa uzima wangu. 2 Uliyenipa usiku kulala ni mzima, nakuomba sasa, Mungu, unilinde mchana. 3 Nilinde majaribuni, kwani sina nguvu, hivi leo maovuni uwe ngao yangu! 4 Katika maneno yangu nisiseme uongo, macho yako, Bwana Mungu, yanitunze mimi! 5 Nija yangu nipitayo wewe uwe nami, kila niendako leo uwe kiongozi! Languages: Swahili

Pages


Export as CSV