Author: P. F. Hiller, 1699-1769 Hymnal: Mwimbieni Bwana #65 (1988) Topics: Epifania, Mission Lyrics: 1 Mfalme ni Yesu pekee,
wote wanamwangukia,
watawalishwa na Mungu.
Ndimi zote ziungame
Yesu ni mfalme pekee,
atukuzwe popote.
2 Mfalme mkubwa,
watu wako
wakutii, wanakusifu.
Yesu apita wafalme,
yeye ndiye mkubwa sana,
apenda kuwakomboa,
kwani ndiye Mwokozi.
3 Enyi watu mpeni mioyo,
mnaohuzunika njooni;
wakiwa semeni naye,
kwani vyote aviweza.
Awagawia uzima
wanaomngoja yeye.
4 Kama wataka uzima,
nenda kwake, acha soni,
yeye anakungojea.
Amejitoa mwenyewe,
wewe upate kurithi,
mbingu ni yako sasa.
5 Nimsifuje Yesu Kristo
mimi vumbi, mimi jivu?
Nasema: Nitamtangaza
Kristo Yesu ndiye Bwana!
Na tumpende, tumheshimu
sifa zote zampasa. Languages: Swahili
Mfalme ni Yesu pekee