1 Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.
Refrain:
Yesu nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi
Nakujia.
2 Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi. [Refrain]
3 Nina haja nawe,
Kila hali,
Maisha ni bure,
Ukiwa mbali, [Refrain]
4 Nina haja nawe,
Nifundishe
Na ahadi zako
zitimize. [Refrain]
5 Nina haja nawe,
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote. [Refrain]
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #275