1 Uliyesulibishwa,
Mtakatifu Bwanangu,
uwe ngao shidani,
uniombee mimi.
Uliyesulibishwa,
Mtakatifu Bwanangu!
2 Wongofu sina hata,
niondolee makosa.
Mwovu akinishtaki,
nasumbuka rohoni.
Wongofu sina hata,
niondolee makosa.
3 Wewe tu nipokee,
nakukimbilia wee.
Hata nifanye bidii,
nikatoe machozi.
Wewe tu nipokee,
nakukimbilia wee.
4 Uwe ngao shidani,
niombee na mimi!
Hapa nikiumizwa,
saa ya mwisho ikija:
Uwe ngao shidani,
niombee na mimi!
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #84