Instance Results

Topics:kuzaliwa+kwa+yesu
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 21 - 30 of 33Results Per Page: 102050
TextPage scan

Njooni wachungaji Betlehemu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #20 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Njooni wachungaji Betlehemu! Lyrics: 1 Njooni wachungaji Betlehemu! Njooni kumtazama mtoto mzuri. Mwana wa Mungu amezaliwa. Baba amtuma awakoboe. Msiogope! 2 Twende Betlehemu tuone tulivyoambiwa na malaika. Tuyaonayo tutatangaza na kutukuza kwa nyimbo nzuri. Haleluya! 3 Kweli malaika wametangaza Furaha kubwa kwa wachungaji. Sasa popote patengenezwe, na watu wote watapendezwa. Furahini! Languages: Swahili
TextPage scan

Msifuni Mungu, Wakristo

Author: N. Hermann, karibu 1480-1561 Hymnal: Mwimbieni Bwana #23 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Msifuni Mungu, Wakristo, aliyetukuka, atufungulia mbingu kumtoa mwanawe, kumtoa mwanawe. 2 Atokaye kifuani pa Mungu Babaye, alal sasa Mtoto mtupu maskini, mtupu, maskini. 3 Anyonya kwa mama yake, maziwa chakula, kwa kweli anatulisha chakula cha mbingu, chakula cha mbingu. 4 Ageuza hali yake, avaa mwili wetu, na sisi anatuvika uzima wa Mungu, uzima wa Mungu. 5 Akawa mtumwa, na mimi naitwa kibwana, niwe nduguye na mtoto wake Mungu Baba, wake Mungu Baba. Languages: Swahili
TextPage scan

Mungu ni wa utukufu

Author: Ch. Wesley Hymnal: Mwimbieni Bwana #25 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Mungu ni wa utukufu panapo mbinguni juu, na kwao wampendezao duniani raha kuu. Sikieni nchi zote huko mjini Betlehemu: Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima, Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima. 2 Watu na malaika wote wanamtukuza Yesu, ashukaye toka mbingu kuwa kama maskini. Akaacha enzi yake, akavaa unyenyekevu Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima, Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima. 3 Asifiwe Mwana Mungu na Mwokozi wa watu, mleta mwanga na uzima Yesu mshinda kuzimu, mfalme wa utengemano huko mjini Betlehemu. Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima, Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima. Languages: Swahili

Tumezaliwa Mtoto

Author: H. Mavula Hymnal: Mwimbieni Bwana #38 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili
Text

Mjini mwake Daudi

Author: C. F. Alexander, 1823-95 Hymnal: Mwimbieni Bwana #43 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Mjini mwake Daudi Bandani mwa wageni Mtoto alizaliwa Na mamaye maskini Mariamu ni mama Yesu mwanawe mwema. 2 Yesu akawa mbinguni Akatoka enzini Hakukaribishwa chini Akalazwa horini Akaja kimaskini Kuketi duniani. 3 Siku za Ujana wake Akimheshimu mama Na kumtii katika yote Kama alivyosema Kila mwana na awe Mtii kama yeye. 4 Amekuwa hata sasa Kielelezo chetu Alikuwa na unyonge Kama unyonge wetu Kucheka na kulia Ni kama sisi sote. 5 Tutamwona waziwazi Ndiyo ahadi yake Sasa aketi mbinguni Katika enzi yake Sote na tumwandame Kwani ni Mfalme wetu. Languages: Swahili
TextPage scan

Amezaliwa mtoto

Hymnal: Mwimbieni Bwana #27 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Amezaliwa mtoto mjini Betlehemu. Nimemchagua yeye, niwe mali yake! Oye, oye, niwe mali yake! 2 Nataka kuingia pendoni mwake yee na kumtolea moyo hata vyangu vyote, Oye, oye, hata vyangu vyote. 3 Kwa moyo wote safi nataka kumpenda shidani, furahani hata hila wasaa. Oye, oye, hata kila wasaa. 4 Unikubali hivyo, naomba kabisa Nikuishie wewe, Leo na daima! Oye, oye, leo na daima! Languages: Swahili
TextPage scan

Siku ya furaha popote

Hymnal: Mwimbieni Bwana #29 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Siku ya furaha popote, sauti za kusifu zavuma. Duniani, nyumbani nyimbo za furaha kuu: Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma. 2 Siku ya furaha popote sauti za kusifu zavuma. Azaliwa Mesiya kwetu duniani; tulio wa gizani tuwe wa mwanga: Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma. 3 Siku ya furaha popote Sauti za kusifu zavuma. Walimwengu wakubwa hata wadogo watangaza kwa shangwe: Tunaye Kristo! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma. Languages: Swahili

Tumshukuru, tumsifu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #52 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Ulimwenguni pote

Author: H. Held, 1620-1659 Hymnal: Mwimbieni Bwana #24 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Ulimwenguni pote asifiwe Mungu mkuu amemtuma Mwokozi, wakosaji wapone. 2 Zamani wazee wale wameona hamu kuu, waondoshwe makosa na kumpata Mwokozi. 3 Abahamu, Yakobo na watu wa Sayuni walimngojea sana, sasa ametujia. 4 Karibu mponya wangu niondolee woga. Ujitengenezee njia moyoni mwangu. 5 Safisha nyumba yako umfukuze Shetani, yule nyoka wa kale. Nikutumikie wee! Languages: Swahili
TextPage scan

Nchi, mbingu furahi

Hymnal: Mwimbieni Bwana #26 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Nchi, mbingu furahi! Lyrics: 1 Nchi, mbingu furahi! Haleluya! Amekuja Mwokozi, Haleluya! Mwana wake Mungu amekuja kwetu, amekuja kwetu. 2 Toka shina la Yese, Haleluya! Tawi limechipuka, Haleluya! Mwana wake Mungu amekuja kwetu, amekuja kwetu. 3 Neno lake Mwenyezi, Haleluya! Limekuja duniani, Haleluya! Mwana wake Mungu amekuja kwetu, amekuja kwetu. Languages: Swahili

Pages


Export as CSV