Instance Results

Topics:kuzaliwa+kwa+yesu
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 1 - 10 of 33Results Per Page: 102050
TextPage scan

Umati wa Yesu

Author: John F. Wade, c.1711-1786 Hymnal: Mwimbieni Bwana #18 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Umati wa Yesu, njooni kwa furaha Lyrics: 1 Umati wa Yesu, njooni kwa furaha msikie habari ya sikukuu! Mwana wa Mungu azaliwa kwetu. Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! 2 Mbinguni malaika wamwimbia wote na wote wakaao kwake Mungu. Mungu ni mkuu, aliyetupenda Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! 3 Tumsifu Mwokozi Yesu siku zote, aliyezaliwa kwetu leo. Anatujia atufurahishe. Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! Languages: Swahili
TextPage scan

Njooni, tumheshimu Yesu

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #12 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Njooni, tumheshimu Yesu, tumtolee sifa zetu, tumwimbie kwa furaha, sisi watu wa Yesu. 2 Baba amemtuma Mwana atuletee uzima, utakaopewa watu wenye shida na kufa. 3 Moyo wake watupenda kwa upendo amekuja, aokoe wenye dhambi wasishindewe na mwovu. 4 Nuru imetutokea, Yesu akiponda kichwa cha adui wetu mkali anayetudanganya. 5 Tutabarikiwa kweli, tukishika neno hili, tukimsifu Bwana Yesu kwa vinywa na mioyo. 6 Mwana mzuri Bwana Yesu, twakuomba tupeleke pale wakuimbiapo malaika nyimbo nzuri. Languages: Swahili
TextPage scan

Tunakuamkia Yesu

Author: M. Luther, 1483-1546 Hymnal: Mwimbieni Bwana #16 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Tunakuamkia Yesu tunakupa pongezi. Umezaliwa kikiwa, malaika wakuabudu, Uwe nasi! 2 Mwana wa Mungu wa pekee, yeye ni mgeni wetu. Anajiunga na sisi Mfalme wa kale na kale! Uwe nasi! 3 Ashikaye ulimwengu ashikwa na Maria! Ni mtoto mdogo na mchanga! Tena ni Bwana wa mbingu! Uwe nasi! 4 Nuru ya milele aja kuleta mwanga wake. Aondoa giza lote; tuwe watoto wa mwanga. Uwe nasi! 5 Kwetu akawa maskini kwa kutuhurumia, tupate mali ya mbingu, tuwe watoto wa Mungu. Uwe nasi! 6 Amefanya haya yote kwa kuwa atupenda. Kwa hiyo fuahini tu na tumshukuru daima! Uwe nasi! Languages: Swahili
Page scan

Yesu mtoto mzuri

Author: E. M. Arndt Hymnal: Mwimbieni Bwana #22 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili

Tumepata Mwokozi

Author: Y. Chambile; F. de Zwart Hymnal: Mwimbieni Bwana #40 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Tumepata Mwokozi sasa Bwana Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Tuimbe na kusifu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #17 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Tuimbe na kusifu kwa nyimbo za furaha: Yesu Bwana wetu amezaliwa leo zizini Betlehemu, furaha ya mioto. Mponya na Mwokozi, tunakusifu. 2 Nakutamani sana, uliyetoka juu. Ee Mowokozi mwema tuliza moyo wangu, unipe neema yako, Mtoto wa huruma. Univute juu, univute juu. 3 Rehema zake Mungu ni nyingi, alimtuma Mwana wake Yesu, awakomboe watu, atufanyie njia, tufike tena kwetu. Kwetu ni kwa Mungu, kwetu kwa Mungu. 4 Na watu wakaao katika giza wote wanakungojea wewe Mowokozi wetu, na kukufurahia uliyetukomboa. Yesu Bwana wetu twakutukuza. Languages: Swahili
TextPage scan

Salamu, Yesu Bwanangu

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #13 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Salamu, Yesu Bwanangu wewe uzima wangu. Nimekujia, naleta vyote ulivyonipa: Ni moyo na nwili wangu, hata na mawazo yangu ndiyo heshima yangu. 2 Umezaliwa Bwanangu kwa ajili ya mimi; umenipenda kabisa, umenipa wokovu. Tangu mimi sijaumbwa umenitengenezea Ukombozi wa moyo. 3 Uvuli mzito wa mauti ulinifunikiza: Umenitokea jua, waniangaza moyo. Wewe Bwana umenipa nuru, raha na uzima. Nakushukuru Bwana. Languages: Swahili
TextPage scan

Natoka leo mbinguni

Author: M. Luther, 1483-1546 Hymnal: Mwimbieni Bwana #11 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Natoka leo mbinguni naleta habari njema habari yenye furaha kwa ninyi na watu wote. 2 "Amezaliwa mtoto na mwanamwali Maria, ni mtoto mzuri na mwema, awaletea furaha." 3 Ni Yesu, Mwana wa Mungu, Mwokozi wa ulimwengu, Atakayekuondoa makosa yote na shida. 4 Awapa wote wokovu uliowek wa na Mungu mkae nanyi mbinquni pamoja nasi milele. 5 Alama yenu iwe hii: Zizini mtoto maskini aliyevik wa viguo, naye ni Bwana wa mbingu. 6 Tumsifuni sisi sote, tuwafuate wachunga, tuyaone yale makuu, tuliyopewa na Mungu. 7 Yesu unipendezaye, ugeuze moyo wangu, uwe nyumba yako nzuri, nisikuache daima. 8 Tumsifu Bwana wa mbingu, aliyemtoa Mwanawe. Tumwimbie kwa furaha pamoja nao malaika. Languages: Swahili

Sote tufurahi

Author: Wilson Kyakajumba Hymnal: Mwimbieni Bwana #36 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Refrain First Line: Sasa yametimia Languages: Swahili

Tushangilie sote

Author: Mudimi Ntandu Hymnal: Mwimbieni Bwana #39 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili

Pages


Export as CSV