Instance Results

Topics:kuteswa+na+kufa+kwa+yesu
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 1 - 10 of 24Results Per Page: 102050
TextPage scan

Yesu, kuteswa kwako

Author: S. V. Birken, 1626-1681 Hymnal: Mwimbieni Bwana #82 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Yesu, kuteswa kwako nitakufikiri. Nipe kwa shauri hili roho na mbaraka. Moyo wangu uone hali yako Yesu, jinsi ulivyoteswa kwa ajili yetu. 2 Moyo wangu uone taabu yako kubwa, maumivu, mapigo, na kuwambwa mtini, taji lako la miiba tena misumari, iliyokuumiza, hata kufa kwako. 3 Nikitazama yote yaliyokutesa, nifikiri sababu na maana yake. Sababu ndio mimi na makosa yangu: umepata mateso, nipate huruma. 4 Yesu unifundishe nijute kwa moyo; nisikuzidishie shida na uchungu. Nisiweze kupenda yaliyokutesa: nataka kuyaacha na kukufuata. Languages: Swahili
TextPage scan

Nakusalimu kichwa

Author: Bernhard V. Clairvaux, 1091-1153; Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #78 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nakusalimu kichwa kilichojaa damu, kilichovikwa taji la miiba mikubwa, kilichopata enzi kwa Mungu mbinguni, kitukanwacho sasa matusi makali. 2 Naona uso wako watemewa mate, heshima yako yote imeondolewa. Mwanga wa macho yako wazimika sasa. Aliyekuharibu hivi, ndiye nani? 3 Mateso yako Bwana, yanipasa mimi. Wewe waadhibishwa kwa ajili yangu. Hukumu unapata iliyonipasa. Bwanangu nakuomba, unihurumie! 4 Na mimi nasimama msalabani pako; niwe karibu kwako utoapo roho; ukiugua sana kwa teso la kufa, nitakushika Bwana kwa moyo wa pendo. 5 Bwana nayashukuru masumbaku yako, sababu ya kuteswa na kufa kuchungu. Wewe umenishika, nami nakushinka, mwisho nitakufia uliyenifia. 6 Moyo unaposhikwa na woga wa kufa, usiniache Bwana katika vita hii. Siku ya kufa kwangu unisaidie, kufa kwako kuchungu kutaniokoa. 7 Niwie kama ngao nitakapokufa, nione uso wako katika uchungu. Ndipo nikutazame nikukumbatie! Anayekufa hivi afa kwa amani. Languages: Swahili
TextPage scan

Ni damu idondokayo

Author: W. Cowper, 1731-1800 Hymnal: Mwimbieni Bwana #90 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ni damu idondokayo mwlini mwa Yesu, wakosaji wakioga, husafishwa kweli. Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! 2 Ilimpatia wokovu mwizi kule mtini; nami nisiyemtafuta, inanisafisha. Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! 3 Na shaushi aliyuemlinda Yesu akiteswa, naye akamshuhudia: Ni mwana wa Mungu! Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! 4 Nipe ulimi mpya Yesu wa kukuimi mpya Yesu w kukuimbia, Babayo tutamtukuza. jina lake pekee. Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! Languages: Swahili
Text

Bwana Yesu alikufa

Hymnal: Mwimbieni Bwana #94 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Bwana Yesu alikufa kwa sababu yetu sisi, alipata duniani maumivu mengi sana. 2 Bustanini akiomba akafadhaika kabisa. Jasho lake kama damu nchini ikadondoka. 3 Wayuda wakamwendea, wakamshika, wakamfunga. Na rafiki zake wote wakimbia, wkamwacha. 4 Na wale wakampeleka barazani kumhukumu. Wamhukumu yule mfalme, atakayewahukumu. 5 Wakamfyosa, wakampiga, wakampeleka Golgota. Kule wakamwamba mtini, kwa misumari kumkaza. 6 Kukawa na giza huko, na nchi ikatetemeka. Watu walioko wote, wakaona woga mwingi. 7 Na saa tisa ikifika Yesu apaza sauti kuu, kwamba: Yamemalizika; mara akakata roho. 8 Askari wakamwendea, wakamwona amekufa. Nao wakamchoma mkuki; ukapenya moyo wake. 9 Damu yaki ikatoka, yakatoka maji tena, Maji, damu iwezago kuosha uchafu wote. 10 Na watu wema wamshusha, wamfunga katika sanda, wakamweka kaburini, na penye mlango jiwe kuu. 11 Siku ya tatu atoka Yesu Kristo kuzimuni, alivyotangaza kwanza. Ye mzima hata milele! Languages: Swahili
TextPage scan

Nataka kusimama

Author: E. C. Clephane, 1830-1869 Hymnal: Mwimbieni Bwana #87 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nataka kusimama chini ya msalaba, kama kivuli cha mwamba wakati wa mchana, kama ni maji nyikani, kambi safarini, na hapa nitapumzika, kwani jua kali. 2 Mahali pema sana chini ya msalaba, kwani hapo waoneka upendo wa Yesu. Yakobo alivyoona ndotoni zamani, mti Yesu aliowambwa, ni ngazi kwa Mungu. 3 Juu ya msalaba huo Yesu alikufa. Alikufa tuokoke, tuliopotea. Ninastaajabu kabisa ni mambo mawili: kwake Yesu ni upendo, kwangu mimi kosa! 4 Wataka kuonana na Yesu mbinguni, yakupasa kukaa kwanza chini ya mti huo. Ni kweli siku chache tu mateso na shaka. Halafu pasipo mwisho furaha kwa Bwana! Languages: Swahili
Text

Yesu alitufia

Hymnal: Mwimbieni Bwana #98 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Yesu alitufia, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 2 Sisi watu wabaya, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 3 Walimchezea Bwana, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 4 Wakamvua mavazi, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 5 Aliteswa Golgotha, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 6 Kasema imekwisha, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 7 Hakushindwa na kifo, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 8 Katoka kaburini, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 9 Kafufuka kwa wafu, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 10 Ndiye Mwokozi wetu, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 11 Ataishi milele, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. Languages: Swahili
TextPage scan

Nimshangilie Bwana wangu

Author: Ph. Bliss Hymnal: Mwimbieni Bwana #83 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nimshangilie Bwana wangu na kumwimbia mkombozi, katukomboa msalabani, nisifu pendo lake kuu. Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 2 Tumsifu yeye mponya wetu katika ulimwengu huu, kutupatanisha na Baba walio wakosaji tu. Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 3 Katuletea mwanga wake, tulikaa katika giza, wokovu ukaonekana, kamshinda mwovu, ni shujaa! Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 4 Na tumtukuze Bwana wetu, tumtumikie kwa bidii, na atawale apendavyo, na sisi sote tutamtii! Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! Languages: Swahili

Wakristo twabeba nini?

Author: Z. D. Mzengi Hymnal: Mwimbieni Bwana #95 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Ukiwa na ubaya

Hymnal: Mwimbieni Bwana #91 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ukiwa na ubaya umwambie Bwana! Ukishindana nao, atakutakasa. Damu aliyotoa, ndiyo itoshayo, kuosha wakosaji, hata wewe vivyo. 2 Vilevile na moyo umtolee Bwana! Ndivyo vipaji vema vinavyompendeza. Kwani sisi wenyewe alitukomboa, akiuawa yeye kwa kuwambwa mtini. 3 Hata viwe vichache umtolee Bwana, vyote tulivyo navyo vimetoka kwake. Vipaji vyako habe yeye hakatai, kidogo kwako wewe, kwake kitazidi! 4 Vitu vya mali nyingi umtolee Bwana! Alitoka mbinguni kusumbuka hapa. Alikufa mwenyewe kwa ajili yako, nawe hutoi chako kwa ajili yake? 5 Wakristo na tutoe shukrani kwa Mungu! Hiyo ndiyo shukrani ya wokovu wetu. Injili yake Kristo, Ienee pote! Kwa ushuhuda wetu watu waokoke. Languages: Swahili
TextPage scan

Ee, watoto njooni

Author: E. G. Woltersdorf Hymnal: Mwimbieni Bwana #86 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ee, watoto njooni, njooni Golgota, mtazameni Yesu aumizwavyo! 2 Mtazameni huko mkamtazame, Sogeeni kwake, ametupenda. 3 Sogeeni kwake, mkamtazame, mioyo iyevuke, mwangukieni! 4 Mioyo imlilie anayeteswa; mzigo wetu mkubwa aukubali. 5 Mzigo wa makosa ya ulimwengu. Mpeni nanyi nyote mioyo yenu! 6 Apata mshahara, ni kufa kwake; wewe una raha, kwake ni kufa. 7 Ataona enzi ya utukufu. Tuimbe Haleluya na kumshukuru! Languages: Swahili

Pages


Export as CSV