Text: | Tunakuamkia Yesu |
Author: | M. Luther, 1483-1546 |
1 Tunakuamkia Yesu
tunakupa pongezi.
Umezaliwa kikiwa,
malaika wakuabudu,
Uwe nasi!
2 Mwana wa Mungu wa pekee,
yeye ni mgeni wetu.
Anajiunga na sisi
Mfalme wa kale na kale!
Uwe nasi!
3 Ashikaye ulimwengu
ashikwa na Maria!
Ni mtoto mdogo na mchanga!
Tena ni Bwana wa mbingu!
Uwe nasi!
4 Nuru ya milele aja
kuleta mwanga wake.
Aondoa giza lote;
tuwe watoto wa mwanga.
Uwe nasi!
5 Kwetu akawa maskini
kwa kutuhurumia,
tupate mali ya mbingu,
tuwe watoto wa Mungu.
Uwe nasi!
6 Amefanya haya yote
kwa kuwa atupenda.
Kwa hiyo fuahini tu
na tumshukuru daima!
Uwe nasi!
Text Information | |
---|---|
First Line: | Tunakuamkia Yesu |
Title: | Tunakuamkia Yesu |
German Title: | Gelobet seist du, Jesu Christ |
Author: | M. Luther, 1483-1546 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kuzaliwa kwa Yesu |
Notes: | Sauti na wimbo: Gelobet seist du, Jesu Christ, Asili: J. Walther, Wittenberg, 1524, Posaunen Buch, Erster Band #15, Lutheran Book of Worship #48 |