Instance Results

Topics:kuteswa+na+kufa+kwa+yesu
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 1 - 24 of 24Results Per Page: 102050
TextPage scan

Yesu, kuteswa kwako

Author: S. V. Birken, 1626-1681 Hymnal: Mwimbieni Bwana #82 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Yesu, kuteswa kwako nitakufikiri. Nipe kwa shauri hili roho na mbaraka. Moyo wangu uone hali yako Yesu, jinsi ulivyoteswa kwa ajili yetu. 2 Moyo wangu uone taabu yako kubwa, maumivu, mapigo, na kuwambwa mtini, taji lako la miiba tena misumari, iliyokuumiza, hata kufa kwako. 3 Nikitazama yote yaliyokutesa, nifikiri sababu na maana yake. Sababu ndio mimi na makosa yangu: umepata mateso, nipate huruma. 4 Yesu unifundishe nijute kwa moyo; nisikuzidishie shida na uchungu. Nisiweze kupenda yaliyokutesa: nataka kuyaacha na kukufuata. Languages: Swahili
TextPage scan

Nakusalimu kichwa

Author: Bernhard V. Clairvaux, 1091-1153; Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #78 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nakusalimu kichwa kilichojaa damu, kilichovikwa taji la miiba mikubwa, kilichopata enzi kwa Mungu mbinguni, kitukanwacho sasa matusi makali. 2 Naona uso wako watemewa mate, heshima yako yote imeondolewa. Mwanga wa macho yako wazimika sasa. Aliyekuharibu hivi, ndiye nani? 3 Mateso yako Bwana, yanipasa mimi. Wewe waadhibishwa kwa ajili yangu. Hukumu unapata iliyonipasa. Bwanangu nakuomba, unihurumie! 4 Na mimi nasimama msalabani pako; niwe karibu kwako utoapo roho; ukiugua sana kwa teso la kufa, nitakushika Bwana kwa moyo wa pendo. 5 Bwana nayashukuru masumbaku yako, sababu ya kuteswa na kufa kuchungu. Wewe umenishika, nami nakushinka, mwisho nitakufia uliyenifia. 6 Moyo unaposhikwa na woga wa kufa, usiniache Bwana katika vita hii. Siku ya kufa kwangu unisaidie, kufa kwako kuchungu kutaniokoa. 7 Niwie kama ngao nitakapokufa, nione uso wako katika uchungu. Ndipo nikutazame nikukumbatie! Anayekufa hivi afa kwa amani. Languages: Swahili
TextPage scan

Ni damu idondokayo

Author: W. Cowper, 1731-1800 Hymnal: Mwimbieni Bwana #90 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ni damu idondokayo mwlini mwa Yesu, wakosaji wakioga, husafishwa kweli. Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! 2 Ilimpatia wokovu mwizi kule mtini; nami nisiyemtafuta, inanisafisha. Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! 3 Na shaushi aliyuemlinda Yesu akiteswa, naye akamshuhudia: Ni mwana wa Mungu! Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! 4 Nipe ulimi mpya Yesu wa kukuimi mpya Yesu w kukuimbia, Babayo tutamtukuza. jina lake pekee. Bwana wangu, Mungu wangu, u uzimawangu, umekutanana kufa kwa ajili yangu! Languages: Swahili
Text

Bwana Yesu alikufa

Hymnal: Mwimbieni Bwana #94 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Bwana Yesu alikufa kwa sababu yetu sisi, alipata duniani maumivu mengi sana. 2 Bustanini akiomba akafadhaika kabisa. Jasho lake kama damu nchini ikadondoka. 3 Wayuda wakamwendea, wakamshika, wakamfunga. Na rafiki zake wote wakimbia, wkamwacha. 4 Na wale wakampeleka barazani kumhukumu. Wamhukumu yule mfalme, atakayewahukumu. 5 Wakamfyosa, wakampiga, wakampeleka Golgota. Kule wakamwamba mtini, kwa misumari kumkaza. 6 Kukawa na giza huko, na nchi ikatetemeka. Watu walioko wote, wakaona woga mwingi. 7 Na saa tisa ikifika Yesu apaza sauti kuu, kwamba: Yamemalizika; mara akakata roho. 8 Askari wakamwendea, wakamwona amekufa. Nao wakamchoma mkuki; ukapenya moyo wake. 9 Damu yaki ikatoka, yakatoka maji tena, Maji, damu iwezago kuosha uchafu wote. 10 Na watu wema wamshusha, wamfunga katika sanda, wakamweka kaburini, na penye mlango jiwe kuu. 11 Siku ya tatu atoka Yesu Kristo kuzimuni, alivyotangaza kwanza. Ye mzima hata milele! Languages: Swahili
TextPage scan

Nataka kusimama

Author: E. C. Clephane, 1830-1869 Hymnal: Mwimbieni Bwana #87 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nataka kusimama chini ya msalaba, kama kivuli cha mwamba wakati wa mchana, kama ni maji nyikani, kambi safarini, na hapa nitapumzika, kwani jua kali. 2 Mahali pema sana chini ya msalaba, kwani hapo waoneka upendo wa Yesu. Yakobo alivyoona ndotoni zamani, mti Yesu aliowambwa, ni ngazi kwa Mungu. 3 Juu ya msalaba huo Yesu alikufa. Alikufa tuokoke, tuliopotea. Ninastaajabu kabisa ni mambo mawili: kwake Yesu ni upendo, kwangu mimi kosa! 4 Wataka kuonana na Yesu mbinguni, yakupasa kukaa kwanza chini ya mti huo. Ni kweli siku chache tu mateso na shaka. Halafu pasipo mwisho furaha kwa Bwana! Languages: Swahili
Text

Yesu alitufia

Hymnal: Mwimbieni Bwana #98 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Yesu alitufia, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 2 Sisi watu wabaya, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 3 Walimchezea Bwana, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 4 Wakamvua mavazi, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 5 Aliteswa Golgotha, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 6 Kasema imekwisha, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 7 Hakushindwa na kifo, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 8 Katoka kaburini, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 9 Kafufuka kwa wafu, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 10 Ndiye Mwokozi wetu, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. 11 Ataishi milele, Tumshukuru! Tumshukuru Bwana wetu; Tumshangilie Yesu Mwokozi. Languages: Swahili
TextPage scan

Nimshangilie Bwana wangu

Author: Ph. Bliss Hymnal: Mwimbieni Bwana #83 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Nimshangilie Bwana wangu na kumwimbia mkombozi, katukomboa msalabani, nisifu pendo lake kuu. Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 2 Tumsifu yeye mponya wetu katika ulimwengu huu, kutupatanisha na Baba walio wakosaji tu. Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 3 Katuletea mwanga wake, tulikaa katika giza, wokovu ukaonekana, kamshinda mwovu, ni shujaa! Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! 4 Na tumtukuze Bwana wetu, tumtumikie kwa bidii, na atawale apendavyo, na sisi sote tutamtii! Haya mwimbieni Yesu, amekubali mateso, katukomboa msalabani, tusifu pendo lake kuu! Languages: Swahili

Wakristo twabeba nini?

Author: Z. D. Mzengi Hymnal: Mwimbieni Bwana #95 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Ukiwa na ubaya

Hymnal: Mwimbieni Bwana #91 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ukiwa na ubaya umwambie Bwana! Ukishindana nao, atakutakasa. Damu aliyotoa, ndiyo itoshayo, kuosha wakosaji, hata wewe vivyo. 2 Vilevile na moyo umtolee Bwana! Ndivyo vipaji vema vinavyompendeza. Kwani sisi wenyewe alitukomboa, akiuawa yeye kwa kuwambwa mtini. 3 Hata viwe vichache umtolee Bwana, vyote tulivyo navyo vimetoka kwake. Vipaji vyako habe yeye hakatai, kidogo kwako wewe, kwake kitazidi! 4 Vitu vya mali nyingi umtolee Bwana! Alitoka mbinguni kusumbuka hapa. Alikufa mwenyewe kwa ajili yako, nawe hutoi chako kwa ajili yake? 5 Wakristo na tutoe shukrani kwa Mungu! Hiyo ndiyo shukrani ya wokovu wetu. Injili yake Kristo, Ienee pote! Kwa ushuhuda wetu watu waokoke. Languages: Swahili
TextPage scan

Ee, watoto njooni

Author: E. G. Woltersdorf Hymnal: Mwimbieni Bwana #86 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ee, watoto njooni, njooni Golgota, mtazameni Yesu aumizwavyo! 2 Mtazameni huko mkamtazame, Sogeeni kwake, ametupenda. 3 Sogeeni kwake, mkamtazame, mioyo iyevuke, mwangukieni! 4 Mioyo imlilie anayeteswa; mzigo wetu mkubwa aukubali. 5 Mzigo wa makosa ya ulimwengu. Mpeni nanyi nyote mioyo yenu! 6 Apata mshahara, ni kufa kwake; wewe una raha, kwake ni kufa. 7 Ataona enzi ya utukufu. Tuimbe Haleluya na kumshukuru! Languages: Swahili
TextPage scan

Mwokozi wangu umekosa nini

Author: J. Heermann, 1585-1647 Hymnal: Mwimbieni Bwana #77 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mwokozi wangu, umekosa nini? Lyrics: 1 Mwokozi wangu, umekosa nini? Wahukumiwa kama mwuaji. Umeshtakiwa makosa mangapi uliyotenda? 2 Wapigwa sana, miiba taji lako, umetemewa mate, watukanwa, wanyweshwa nyongo, tena siki kali, wasulibishwa! 3 Sababu gani unateswa hivi? Makosa yangu yanakuumiza; mateso haya yako yanipasa, mimi mkosaji. 4 Ajabu kubwa sana tendo lako: Mchungaji unateswa kwa ajili ya kondoo, Bwana unawalipia watumwa wako. 5 Tulipokuwa mateka ya mwovu, nawe ukaja ukatukomboa. Twalistahili kufa kwa milele, ukatufia. 6 Mwokozi wangu nifanyeje mimi, niitangaze pote sifa yako? Nakufuata nikutumikie maisha yote. Languages: Swahili
TextPage scan

Roho yangu tua hapa

Author: G. Tersteegen, 1697-1769 Hymnal: Mwimbieni Bwana #85 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Roho yangu tua hapa mlimani pa Golgota, angalia tendo hili, afanyalo mfalme mkuu. Amevutwa na upendo kuacha enzi yake. 2 Yesu alivyotupenda, twaona msalabani, maumivu hata manza ya makosa yampata. Anakaa malali petu, sikia ateswavyo! 3 Kufa kwako kunivute nife pamoja nawe, mwili na mapenzi yangu yakazikwe nawe. Niwe na kutengemana, mwenye pendo la kweli! Languages: Swahili
TextPage scan

Ulimwengu tazama

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #80 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Ulimwengu tazama, Yesu Mwokozi wako asulibiwavyo. Mwenye heshima yote anayavummilia mateso tena matusi. 2 Karibia tazama maungo yake yote yatokavyo damu. Na moyo wake mwema kwa shida na uchungu unaugua vigumu. 3 Nani akupigaye, aliyekufanyia mambo kama haya? Wewe huna makosa kama wengine wote, hujui kosa lolote. 4 Makosa yangu mimi yaliyo kama mchanga, hayahesabiki, ndiyo yakutiayo mateso na uchungu uliyoyavumilia. 5 Mimi nimestahili kulipa haya yote, na kufungwa sana. Mapigo na mateso uliyopata wewe yalitoka kwangu mimi. 6 Umejitwika mzigo ulio mzito sana kuliko jiwe kuu. Wachukua maovu, tupate kuokoka tukae nawe daima! Languages: Swahili
TextPage scan

Mungu tusaidie

Hymnal: Mwimbieni Bwana #99 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Refrain First Line: Kweli kweli ndiye Yesu Lyrics: 1 Mungu tusaidie, Sisi tunaangamia. Nchi imeharibika Na mwovu wake Shetani. Refrain: Kweli kweli ndiye Yesu Aliyewambwa mtini Penye mlima wa Golgotha Aokoe wenye dhambi. 2 Kaonyesha huruma, Wayuda wakasumbua. Wakampiga makofi, Pilato aliamua. [Refrain] 3 Yesu mwenye upendo Alikubali kuuawa, Damu ilimwagika Ili sisi tuokoke. [Refrain] 4 Pale msalabani, Bwana Yesu aliteswa Mzigo wa dhambi zetu Ulimwangukia yeye. [Refrain] 5 Sote na tukumbuke, Kifo cha Mwokozi wetu. Alisema ya kwamba Jililieni wenyewe. [Refrain] 6 Habari zilisemwa, Mahali hapa hayupo, Ona alipokuwa, Jiwe limeondolewa. [Refrain] 7 Ni ajabu kabisa Wingu kuja kumpokea. Habari ilisema Yesu atarudi tena. [Refrain] Languages: Swahili
TextPage scan

Liko neno moja nipendalo

Author: A. Kanpp, 1798-1864 Hymnal: Mwimbieni Bwana #79 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Liko neno moja nipendalo, ni chakula cha moyo; neno hili linanituliza nikipatwa na shida: Kumtazama Bwana wetu pale, atoapo jasho kama damu, akubalipo mzigo, Baba aliomtwika. 2 Siku zote namkumbuka yeye, alivyosulibishwa, akivumilia taabu kimya kama mwana wa kondoo. Nami akanikumbuka mimi, akisema: Yamemalizika! Huko aliniteka, nami niwe mtu wake. 3 Bwana wangu, u mwenye huruma, mimi ni mkosaji tu; nilipokuwapo penye giza wewe ukatokea, ukamtafuta kondoo wako, kabla mimi sijakusikia. Watoa makombozi yanipayo uhuru. 4 Nimi huru lako, Bwana Yesu, wewe ndiwe Bwanangu. Jina lako, bora liung'aze moyo wangu vizuri. Amani yako tukae nayo, siku zangu zote mpaka kufa. Ndivyo ninavyoomba, Bwana unikubali. Languages: Swahili

Mungu ameona tulivyo

Author: Y. Chambile Hymnal: Mwimbieni Bwana #97 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mungu ameona Refrain First Line: Ya kwamba Yesu kaja Languages: Swahili
TextPage scan

Kumbuka Getsemane

Hymnal: Mwimbieni Bwana #88 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Kumbuka Getsemane, asongapo Shetani, Mwokozi ukamwone ateswavyo shambani; nao uchungu wewe, aombapo Kumbuka! 2 Kumbuka barazani ashtakiwapo Yesu; mtazame Bwana huko, walipomhukumia; upate soni wewe, mti wa Yesu Kumbuka! 3 Kumbuka na Golgota alipokufa Bwana. Upaji wa tambiko ameutoa yeye. Kasema: Imekwisha Mti was Yesu Kumbuka! 4 Kumbuka bustanini walipomzika Yesu, kukiwa bado giza. Mfu amekwenda wapi? Amefufuka yeye: Ufufuko Kumbuka! Languages: Swahili
TextPage scan

Mwana kondoo wa Mungu

Author: N. Decius Hymnal: Mwimbieni Bwana #81 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Mwana kondoo wa Mungu unachinjwa msalabani wavumilia sana ujapodharauliwa. Waichukua dhambi, tupate kuokoka. Utuhurumi Yesu. 2 Mwana kondoo wa Mungu unachinjwa msalabani wavumilia sana ujapodharauliwa. Waichukua dhambi, tupate kuokoka. Utuhurumie Yesu. 3 Mwana kondoo wa Mungu unachinjwa msalabani wavumilia sana ujapodharauliwa. Waichukua dhambi, tupate kuokoka. Tutulize mioyo, Yesu. Languages: Swahili
TextPage scan

Unipe nguvu, Bwana

Author: Christian F. Gellert, 1715-1769 Hymnal: Mwimbieni Bwana #93 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Unipe nguvu, Bwana nikumbuke Lyrics: 1 Unipe nguvu, Bwana nikumbuke mateso yako yaliyokupata, kutukoboa tulioanguka katika dhambi. 2 Umemtii Baba mpaka kufa kwako mahali petu ulisulibishwa makosa yetu yalikuwa mengi, umetufia. 3 Wokovu wangu ulinitafuta; nakunangukia Mwokozi wangu, nakushukuru nikiitazama huruma yako. Languages: Swahili
TextPage scan

Mwana knodoo ayalipa

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #75 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mwana kondoo ayalipa Lyrics: 1 Mwana kondoo ayalipa madeni ya dunia. Ayachukua makosa ya wakosaji wote. Aenda na kuugua, anakubali kuchinjwa, furaha aziacha. Wanamhukumu wampiga, wanamukana, wanamtesa, asema: Nakubali. 2 Mwana kondoo ni Mwokozi ni mponya wa mioyo, aliyetumwa na Mungu awakomboe watu Mwanangu, nenda okoa watoto niliotupa, sababu ya makosa. Dhambi zao ni nyingi mno; watolee ukombozi damu na mwili, wako. 3 "Tayari mimi, Babangu, nitwishe nichukue. Maneno uyasemayo nitafuata yote." Pendo hili kubwa sana, lamshika Baba wa mbingu amtoe mwana wake. Pendo hili lina nguvu, linamlaza kaburini aletaye uzima. 4 Sitasahau pendo hili Bwanangu siku zote. Nitakushika daima, kama unishikavyo. Mwanga wa roho ni wewe; roho inapozimia niwie moyo wangu. Na tuagane, Bwanangu, niwe mali yako sasa na halafu mbinguni. Languages: Swahili
TextPage scan

Uliyesulibishwa

Hymnal: Mwimbieni Bwana #84 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu Lyrics: 1 Uliyesulibishwa, Mtakatifu Bwanangu, uwe ngao shidani, uniombee mimi. Uliyesulibishwa, Mtakatifu Bwanangu! 2 Wongofu sina hata, niondolee makosa. Mwovu akinishtaki, nasumbuka rohoni. Wongofu sina hata, niondolee makosa. 3 Wewe tu nipokee, nakukimbilia wee. Hata nifanye bidii, nikatoe machozi. Wewe tu nipokee, nakukimbilia wee. 4 Uwe ngao shidani, niombee na mimi! Hapa nikiumizwa, saa ya mwisho ikija: Uwe ngao shidani, niombee na mimi! Languages: Swahili
TextPage scan

Mwana kondoo wa Mungu waiondoa dhambi

Hymnal: Mwimbieni Bwana #76 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mwana kondoo wa Mungu Lyrics: 1 Mwana kondoo wa Mungu waiondoa dhambi; Tuhurumie. 2 Mwana kondoo wa Mungu waiondoa dhambi; Tuhurumie. 3 Mwana kondoo wa Mungu waiondoa dhambi; Ututulize. Amini. Languages: Swahili
TextPage scan

Njoo msalabani

Hymnal: Mwimbieni Bwana #92 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Njoo msalabani ukilemewa, wewe msafiri! Lyrics: 1 Njoo msalabani ukilemewa, wewe msafiri! Kwenye msalaba utapumzika, ndipo raha. 2 Wamwona mwana kondoo wa Mungu, akichukua mshahara mkuu wa makosa yako, akufia. 3 Yeye asiye mkosaji hata, ahukumiwa. Waona jinsi akupendavyo ewe mdhambi? Languages: Swahili
Text

Mwana kondoo wa Mungu uichukuaye dhambi

Hymnal: Mwimbieni Bwana #96 (1988) Topics: Kuteswa na kufa kwa Yesu First Line: Mwana kondoo wa Mungu Lyrics: 1 Mwana kondoo wa Mungu, Uichukuaye dhambi yote, Mwana kondoo wa Mungu, Uturehemu wakosaji, Mwana kondoo wa Mungu. 2 Mwana kondoo wa Mungu, Uichukuaye dhambi yote, Mwana kondoo wa Mungu, Uturehemu wakosaji, Mwana kondoo wa Mungu. 3 Mwana kondoo wa Mungu, Uichukuaye dhambi yote, Mwana kondoo wa Mungu, Utupe amani yako, Mwana kondoo wa Mungu. Amini. Languages: Swahili

Export as CSV