Instance Results

Topics:kuzaliwa+kwa+yesu
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 1 - 33 of 33Results Per Page: 102050
TextPage scan

Umati wa Yesu

Author: John F. Wade, c.1711-1786 Hymnal: Mwimbieni Bwana #18 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Umati wa Yesu, njooni kwa furaha Lyrics: 1 Umati wa Yesu, njooni kwa furaha msikie habari ya sikukuu! Mwana wa Mungu azaliwa kwetu. Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! 2 Mbinguni malaika wamwimbia wote na wote wakaao kwake Mungu. Mungu ni mkuu, aliyetupenda Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! 3 Tumsifu Mwokozi Yesu siku zote, aliyezaliwa kwetu leo. Anatujia atufurahishe. Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Njooni tumtukuze! Yesu Kristo! Languages: Swahili
TextPage scan

Njooni, tumheshimu Yesu

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #12 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Njooni, tumheshimu Yesu, tumtolee sifa zetu, tumwimbie kwa furaha, sisi watu wa Yesu. 2 Baba amemtuma Mwana atuletee uzima, utakaopewa watu wenye shida na kufa. 3 Moyo wake watupenda kwa upendo amekuja, aokoe wenye dhambi wasishindewe na mwovu. 4 Nuru imetutokea, Yesu akiponda kichwa cha adui wetu mkali anayetudanganya. 5 Tutabarikiwa kweli, tukishika neno hili, tukimsifu Bwana Yesu kwa vinywa na mioyo. 6 Mwana mzuri Bwana Yesu, twakuomba tupeleke pale wakuimbiapo malaika nyimbo nzuri. Languages: Swahili
TextPage scan

Tunakuamkia Yesu

Author: M. Luther, 1483-1546 Hymnal: Mwimbieni Bwana #16 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Tunakuamkia Yesu tunakupa pongezi. Umezaliwa kikiwa, malaika wakuabudu, Uwe nasi! 2 Mwana wa Mungu wa pekee, yeye ni mgeni wetu. Anajiunga na sisi Mfalme wa kale na kale! Uwe nasi! 3 Ashikaye ulimwengu ashikwa na Maria! Ni mtoto mdogo na mchanga! Tena ni Bwana wa mbingu! Uwe nasi! 4 Nuru ya milele aja kuleta mwanga wake. Aondoa giza lote; tuwe watoto wa mwanga. Uwe nasi! 5 Kwetu akawa maskini kwa kutuhurumia, tupate mali ya mbingu, tuwe watoto wa Mungu. Uwe nasi! 6 Amefanya haya yote kwa kuwa atupenda. Kwa hiyo fuahini tu na tumshukuru daima! Uwe nasi! Languages: Swahili
Page scan

Yesu mtoto mzuri

Author: E. M. Arndt Hymnal: Mwimbieni Bwana #22 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili

Tumepata Mwokozi

Author: Y. Chambile; F. de Zwart Hymnal: Mwimbieni Bwana #40 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Tumepata Mwokozi sasa Bwana Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Tuimbe na kusifu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #17 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Tuimbe na kusifu kwa nyimbo za furaha: Yesu Bwana wetu amezaliwa leo zizini Betlehemu, furaha ya mioto. Mponya na Mwokozi, tunakusifu. 2 Nakutamani sana, uliyetoka juu. Ee Mowokozi mwema tuliza moyo wangu, unipe neema yako, Mtoto wa huruma. Univute juu, univute juu. 3 Rehema zake Mungu ni nyingi, alimtuma Mwana wake Yesu, awakomboe watu, atufanyie njia, tufike tena kwetu. Kwetu ni kwa Mungu, kwetu kwa Mungu. 4 Na watu wakaao katika giza wote wanakungojea wewe Mowokozi wetu, na kukufurahia uliyetukomboa. Yesu Bwana wetu twakutukuza. Languages: Swahili
TextPage scan

Malaika njooni toka juu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #31 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Malaika njooni toka juu! Oye, oye, tazama, tazama mtoto. Imbeni pigeni panda. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria. 2 Kwa sauti kuu mwimbieni! Oye, oye, tazama, tazama mtoto, kwa vinanda na vinubi. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria. 3 Tungenni nyimbo tamu mno, Oye, oye, tazama, tazama mtoto, kupita ndege za anga. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria. 4 Utamu wa nyimbo zenu, Oye, oye, tazama, tazama mtoto, umbembeleze, alale. Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria. 5 Watu na watengemane, Oye, oye, tazama, tazama mtoto, na Mungu tumpe shukrani! Haleluya! Haleluya! Nyimbo za Yesu na Maria. Languages: Swahili
TextPage scan

Salamu, Yesu Bwanangu

Author: Paul Gerhardt, 1607-1676 Hymnal: Mwimbieni Bwana #13 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Salamu, Yesu Bwanangu wewe uzima wangu. Nimekujia, naleta vyote ulivyonipa: Ni moyo na nwili wangu, hata na mawazo yangu ndiyo heshima yangu. 2 Umezaliwa Bwanangu kwa ajili ya mimi; umenipenda kabisa, umenipa wokovu. Tangu mimi sijaumbwa umenitengenezea Ukombozi wa moyo. 3 Uvuli mzito wa mauti ulinifunikiza: Umenitokea jua, waniangaza moyo. Wewe Bwana umenipa nuru, raha na uzima. Nakushukuru Bwana. Languages: Swahili
Text

Mtoto mpenzi lala wee

Hymnal: Mwimbieni Bwana #32 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Mtoto mpenzi lala wee, Mtoto wa mbinguni! Malaika wakupepea ulale kwa raha. Nasi maskini wachunga tunakubembeleza wee. Ulale, lala. Mtoto wee, ulale. 2 Maria kwa upendo mkuu amlaza vizuri. Yosefu akata pumzi ili asimwamshe. Na wanyama wa nyumbani wamenyamaa kabisa: Ulale, lala. Mtoto wee, ulale. 3 Utakapokua Yesu, watakuumiza. Kilimani pa Golgota, watakuua wee. Kwa hiyo sasa lala tu! Kwa raha na utulivu! Ulale, lala. Mtoto wee, ulale. Languages: Swahili
TextPage scan

Natoka leo mbinguni

Author: M. Luther, 1483-1546 Hymnal: Mwimbieni Bwana #11 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Natoka leo mbinguni naleta habari njema habari yenye furaha kwa ninyi na watu wote. 2 "Amezaliwa mtoto na mwanamwali Maria, ni mtoto mzuri na mwema, awaletea furaha." 3 Ni Yesu, Mwana wa Mungu, Mwokozi wa ulimwengu, Atakayekuondoa makosa yote na shida. 4 Awapa wote wokovu uliowek wa na Mungu mkae nanyi mbinquni pamoja nasi milele. 5 Alama yenu iwe hii: Zizini mtoto maskini aliyevik wa viguo, naye ni Bwana wa mbingu. 6 Tumsifuni sisi sote, tuwafuate wachunga, tuyaone yale makuu, tuliyopewa na Mungu. 7 Yesu unipendezaye, ugeuze moyo wangu, uwe nyumba yako nzuri, nisikuache daima. 8 Tumsifu Bwana wa mbingu, aliyemtoa Mwanawe. Tumwimbie kwa furaha pamoja nao malaika. Languages: Swahili
Text

Wacristo furahini

Hymnal: Mwimbieni Bwana #34 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Wakristo furahini Lyrics: 1 Wakristo furahini, furahini sana! Mwaipigiwa leo mbiu yenu njema! Malaika wanaimba huko juu mbinguni, wanaimba vizuri sauti ya kushangaa! wanaimba vizuri sauti ya kushangaa! 2 Hivi wanavyoimba: Furahini nyote! Acheni kuogopa, tazameni nyote kwani amezaliwa Mwokozi wa pekee: ni Bwana Yesu Kristo, Mwana Mungu wetu! ni Bwana Yesu Kristo, Mwana Mungu wetu! 3 Shangilieni nyote na kusikiliza. Wapigieni nyote mbiu na sauti kuu. Mungu katupa sote mtoto wa mbinguni, kwa kutupenda sisi amekuja kwetu. kwa kutupenda sisi amekuja kwetu. Languages: Swahili

Sote tufurahi

Author: Wilson Kyakajumba Hymnal: Mwimbieni Bwana #36 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Refrain First Line: Sasa yametimia Languages: Swahili

Tushangilie sote

Author: Mudimi Ntandu Hymnal: Mwimbieni Bwana #39 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili

Yesu ulale

Author: Mudimi Ntandu Hymnal: Mwimbieni Bwana #42 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili

Bwana Yesu amezaliwa

Author: Boanerge Moshi Hymnal: Mwimbieni Bwana #44 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Bwana Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Siku ya furaha

Author: J. D. Falk, 1786-1826 Hymnal: Mwimbieni Bwana #14 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Siku ya furaha, siku ya uzima Lyrics: 1 Siku ya furaha, siku ya uzima aliyozaliwa Yesu. Tulipotea, Yesu akaja. Furahini, furahimi, Wakristo! Tulipotea, Yesu akaja. Furahini, furahimi, Wakristo! 2 Siku ya furaha, siku ya uzima aliyozaliwa Yesu. Yesu ameshuka, atuokoe. Furahini, furahini, Wakristo! Yesu ameshuka, atuokoe. Furahini, furahini, Wakristo! 3 Siku ya furaha, siku ya uzima aliyozaliwa Yesu. Malaika wote wamsifu Mungu. Furahini, furahini, Wakristo! Malaika wote wamsifu Mungu. Furahini, furahini, Wakristo! Languages: Swahili
Text

Mwema, mwema, mwema ni Bwana

Hymnal: Mwimbieni Bwana #35 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Mwema, mwema, mwema ni Bwana mbinguni, na Lyrics: Mwema, mwema, mwema ni Bwana mbinguni, na utengemano, na utengemano kwa watu wanaompendeza, kwa watu wanaompendeza Mwema ni Bwana mbinguni mwema ni Bwana mbinguni, nchi itengemane, watu wapendezwe, wote wakampendeze Bwana. Mwema, mwema, mwema ni Bwana mbinguni na utengemano kwa watu wanaompendeza, kwa watu wanaompendeza! Scripture: Luke 2:14 Languages: Swahili
TextPage scan

Watoto njooni Betlehemu

Author: Chr. v. Schmidt Hymnal: Mwimbieni Bwana #21 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Watoto njooni Bethlehemu, njooni zizini kuona makuu Mungu aliyotutendea leo, watoto waone furaha kubwa. 2 Twaona Mtoto mzuri hapa, wazee wamtazama, wanafuahi! Wachungaji wote wanamwangukia, malaika wa mbingu wanamwimbia. 3 Pigeni magoti na wachungaji! Wakubwa, wadogo tumnyenyekee! Tuimbe na sisi kwa furaha kuu nyimbo za kumsifu Mwokozi Yesu! 4 Watoka mbinguni utuokoe, waona uchungu sababu yetu, leo wazaliwa mwana kikiwa. Halafu wateswa, unatufia. 5 Twapenda kukupa mioyo yetu, twataka kukutumikia vema. Takasa mioyo ikupendeze, tupate kufika kwako mbinguni. Languages: Swahili
TextPage scan

Mpige mbio, wachungaji

Hymnal: Mwimbieni Bwana #30 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Mpige mbio, wachungaji mpige mbio wote, Chukueni na filimbi na zumari pia. Mpige mbio wote mpige mbio woe Betlehemu kwennya hori waliao ng'ombe. 2 Mumtazame mtoto mzuri aliyezaliwa, na wazazi wake mtoto wako huko naye Ni Yosefu baba na Maria mama, mwanamwali mzuri sana kama malaika juu. 3 Hebu njooni, ee jamani mlete nguo nzuri! Tumlazeni mtoto wetu kwa uzuri wote! Twakubembeleza Wewe mtoto lala! Lala Yesu mpenzi wetu twakubembeleza. Languages: Swahili
TextPage scan

Usiku mtakatifu

Author: J. Mohr, 1792-1848 Hymnal: Mwimbieni Bwana #19 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Usiku mtakatifu! Wengine walala wakeshao ni Yosefu tu na Maria waliomlinda Yesu mwana mzuri Yesu mwana mzuri. 2 Usiku mtakatifu! Wachunga wapewa habari nzuri na malaika, zienezwe popote sasa: Yesu mponya kaja Yesu mponya kaja. 3 Usiku mtakatifu! Siku ya furaha imetuangaza Kimungu tumeupewa ukombozi Kristo amefika Kristo amefika. Languages: Swahili
TextPage scan

Njooni wachungaji Betlehemu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #20 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Njooni wachungaji Betlehemu! Lyrics: 1 Njooni wachungaji Betlehemu! Njooni kumtazama mtoto mzuri. Mwana wa Mungu amezaliwa. Baba amtuma awakoboe. Msiogope! 2 Twende Betlehemu tuone tulivyoambiwa na malaika. Tuyaonayo tutatangaza na kutukuza kwa nyimbo nzuri. Haleluya! 3 Kweli malaika wametangaza Furaha kubwa kwa wachungaji. Sasa popote patengenezwe, na watu wote watapendezwa. Furahini! Languages: Swahili
TextPage scan

Msifuni Mungu, Wakristo

Author: N. Hermann, karibu 1480-1561 Hymnal: Mwimbieni Bwana #23 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Msifuni Mungu, Wakristo, aliyetukuka, atufungulia mbingu kumtoa mwanawe, kumtoa mwanawe. 2 Atokaye kifuani pa Mungu Babaye, alal sasa Mtoto mtupu maskini, mtupu, maskini. 3 Anyonya kwa mama yake, maziwa chakula, kwa kweli anatulisha chakula cha mbingu, chakula cha mbingu. 4 Ageuza hali yake, avaa mwili wetu, na sisi anatuvika uzima wa Mungu, uzima wa Mungu. 5 Akawa mtumwa, na mimi naitwa kibwana, niwe nduguye na mtoto wake Mungu Baba, wake Mungu Baba. Languages: Swahili
TextPage scan

Mungu ni wa utukufu

Author: Ch. Wesley Hymnal: Mwimbieni Bwana #25 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Mungu ni wa utukufu panapo mbinguni juu, na kwao wampendezao duniani raha kuu. Sikieni nchi zote huko mjini Betlehemu: Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima, Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima. 2 Watu na malaika wote wanamtukuza Yesu, ashukaye toka mbingu kuwa kama maskini. Akaacha enzi yake, akavaa unyenyekevu Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima, Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima. 3 Asifiwe Mwana Mungu na Mwokozi wa watu, mleta mwanga na uzima Yesu mshinda kuzimu, mfalme wa utengemano huko mjini Betlehemu. Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima, Kristo amezaliwa, Bwana wetu daima. Languages: Swahili

Tumezaliwa Mtoto

Author: H. Mavula Hymnal: Mwimbieni Bwana #38 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili
Text

Mjini mwake Daudi

Author: C. F. Alexander, 1823-95 Hymnal: Mwimbieni Bwana #43 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Mjini mwake Daudi Bandani mwa wageni Mtoto alizaliwa Na mamaye maskini Mariamu ni mama Yesu mwanawe mwema. 2 Yesu akawa mbinguni Akatoka enzini Hakukaribishwa chini Akalazwa horini Akaja kimaskini Kuketi duniani. 3 Siku za Ujana wake Akimheshimu mama Na kumtii katika yote Kama alivyosema Kila mwana na awe Mtii kama yeye. 4 Amekuwa hata sasa Kielelezo chetu Alikuwa na unyonge Kama unyonge wetu Kucheka na kulia Ni kama sisi sote. 5 Tutamwona waziwazi Ndiyo ahadi yake Sasa aketi mbinguni Katika enzi yake Sote na tumwandame Kwani ni Mfalme wetu. Languages: Swahili
TextPage scan

Amezaliwa mtoto

Hymnal: Mwimbieni Bwana #27 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Amezaliwa mtoto mjini Betlehemu. Nimemchagua yeye, niwe mali yake! Oye, oye, niwe mali yake! 2 Nataka kuingia pendoni mwake yee na kumtolea moyo hata vyangu vyote, Oye, oye, hata vyangu vyote. 3 Kwa moyo wote safi nataka kumpenda shidani, furahani hata hila wasaa. Oye, oye, hata kila wasaa. 4 Unikubali hivyo, naomba kabisa Nikuishie wewe, Leo na daima! Oye, oye, leo na daima! Languages: Swahili
TextPage scan

Siku ya furaha popote

Hymnal: Mwimbieni Bwana #29 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Siku ya furaha popote, sauti za kusifu zavuma. Duniani, nyumbani nyimbo za furaha kuu: Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma. 2 Siku ya furaha popote sauti za kusifu zavuma. Azaliwa Mesiya kwetu duniani; tulio wa gizani tuwe wa mwanga: Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma. 3 Siku ya furaha popote Sauti za kusifu zavuma. Walimwengu wakubwa hata wadogo watangaza kwa shangwe: Tunaye Kristo! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma! Wote sharikieni fuaha yetu, mwanga wa ulimwengu waja toka juu! Siku ya furaha popote, Sauti za kusifu zavuma. Languages: Swahili

Tumshukuru, tumsifu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #52 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili
TextPage scan

Ulimwenguni pote

Author: H. Held, 1620-1659 Hymnal: Mwimbieni Bwana #24 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Ulimwenguni pote asifiwe Mungu mkuu amemtuma Mwokozi, wakosaji wapone. 2 Zamani wazee wale wameona hamu kuu, waondoshwe makosa na kumpata Mwokozi. 3 Abahamu, Yakobo na watu wa Sayuni walimngojea sana, sasa ametujia. 4 Karibu mponya wangu niondolee woga. Ujitengenezee njia moyoni mwangu. 5 Safisha nyumba yako umfukuze Shetani, yule nyoka wa kale. Nikutumikie wee! Languages: Swahili
TextPage scan

Nchi, mbingu furahi

Hymnal: Mwimbieni Bwana #26 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu First Line: Nchi, mbingu furahi! Lyrics: 1 Nchi, mbingu furahi! Haleluya! Amekuja Mwokozi, Haleluya! Mwana wake Mungu amekuja kwetu, amekuja kwetu. 2 Toka shina la Yese, Haleluya! Tawi limechipuka, Haleluya! Mwana wake Mungu amekuja kwetu, amekuja kwetu. 3 Neno lake Mwenyezi, Haleluya! Limekuja duniani, Haleluya! Mwana wake Mungu amekuja kwetu, amekuja kwetu. Languages: Swahili
TextPage scan

Amkeni upesi

Hymnal: Mwimbieni Bwana #28 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Amkeni upesi wachunga kondoo! Malaika washuka, habari watupa: Furaha karibu, Mwokozi aja! 2 Wachungaji njooni, tumtafuteni! Akiwa zizini pigeni filimbi Furaha karibu, Mwokozi aja! 3 Wachungaji hima washika njia. Pamoja wamwona mamaye, babaye. Furaha karibu, Mwokozi aja! 4 Wamjua upesi mtoto wa mbingu. Wapiga magoti kumwimbia nyimbo Furaha karibu, Mwokozi aja! Languages: Swahili

Sauti imetoka mbinguni

Author: B. Mung'ong'o Hymnal: Mwimbieni Bwana #37 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Languages: Swahili
Text

Ilitoka Nuru Kuu

Hymnal: Mwimbieni Bwana #41 (1988) Topics: Kuzaliwa kwa Yesu Lyrics: 1 Ilitoka nuru kuu, Kuliko nuru zote; Na huo wimbo wa juu Wapita nyimbo zote; Ndiyo habari tukufu, Ya Kristo wa utukufu, Awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi, Imanueli. 2 Mwaka huandama mwaka, Wimbo huo na uimbwe; Wapenda kukumbuka, Mzee na wanawe, Ndiyo habari tukufu, Ya Kristo wa utukufu, Awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi, Imanueli. 3 Twafurahi siku hii Ijavyo kila mwaka; Nasi tufanye bidii Huku tukikumbuka, Niyo habari tukufu, Ya Kristo wa utukufu, Awajia wapole; Ni Mungu pamoja na sisi, Imanueli. Languages: Swahili

Export as CSV